THE DREAM STUDIOS

wambura babu log

DARDYS FASHION

DARDYS FASHION

Sunday, 4 January 2015

Matanki ya kuhifadhi mafuta yachomwa moto Libya

Moto ukiwaka kwenye moja ya matanki ya mafuta Libya
Moto ukiwaka kwenye moja ya matanki ya mafuta Libya
Televisheni za ndani nchini Libya zinaripoti kuwa wafanyakazi wa idara ya zima moto  wamezima moto katika matanki kadhaa ya kuhifadhi  mafuta kwenye bandari ya Sidra Jumatatu lakini maeneo mengine bado yanawaka moto.
Serikali inayotambulika kimataifa iliyopo  katika mji wa Tobruk na ushirika wa wanamgambo wa kiislamu katika mji mkuu wa Tripoli wanashutumiana  kwa kushambulia maeneo hayo ya matanki ya kuhifadhi  mafuta.
Mioto katika eneo linalojulikana kama “ Oil triangle” nchini Libya umesababisha bei ya mafuta duniani kupanda kidogo  na kuzusha hofu ya kutokea uharibifu mkubwa wa kimazingira.
Televisheni za Libya zinaripoti kwamba wafanyakazi wa idara ya zima moto walifanikiwa kuzima moto katika baadhi ya matanki ya kuhifadhi mafuta, lakini vyombo vingine vya habari vya kiarabu vimeonesha picha ya moto mkubwa unaondelea kuwaka na kusababisha moshi mkubwa hewani .
Maafisa nchini Libya wameomba msaada kutoka  Italy kuzima moto huo lakini serikali ya Italia imesema itafanya hivyo endapo tu ghasia za  ushirika wa wanamgambo wa kiislamu mjini  Tripoli na vikosi vinavyoitii serikali kwenye mji wa Tobruk zitakapositishwa.
Mtaalamu wa masuala ya mafuta nchini Libya, Tareq Ibrahim  ameiambia televisheni ya serikali kwamba moto umesababisha uharibifu mkubwa katika uchumi wa nchi.
Amesema uharibifu umeigharimu Libya  dola milioni 180. Amekadiria kuwa itachukua karibu miaka mitatu kukarabati au kujenga tena matanki hayo.
Uuzaji nje  wa mafuta kutoka pande zote za sidra na bandari ya karibu ya Ras Lanouf ulisitishwa wiki chache zilizopita baada ya serikali ya Omar al Hassy  ilipojitangazia utawala mjini Tripoli kuapa kuchukua udhibiti wa vinu vya  mafuta kutoka serikali inayotambuliwa kimataifa ya Abdullah al- Thani.
Mashahidi wanasema moto katika matanki ya kuhifadhi mafuta  ulianza wakati ushirika wa wanamgambo wa Farj ulipofyatua roketi  huko sidra wiki iliyopita katika jaribio lililoshindikana la kuuchukua mji huo.
Msemaji wa wanamgambo wa Farj alidai wapinzani wao walihusika na uchomaji moto huo.
Msemaji wa wanamgambo Islamil Shoukri pia alisema ndege za kivita za Libya zinazotii serikali ya Thani na kamanda mstaafu wa kijeshi  khalifa Hafter walipiga  mabomu bandari za Sidra na Ben Jawad siku ya  Jumatatu, na kusababisha majeruhi.
VOA haikuweza kupata uthibitisho huru wa madai hayo.