
Klabu ya Crystal Palace imemtangaza rasmi Alan Pardew kama meneja wake mpya kwa kumpatia mkataba wa miaka mitatu na nusu.
Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Newcastle United alikuwepo uwanjani
siku ambayo klabu yake hiyo mpya ilikua ikiminyana na Aston Villa
kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 0:0 siku ya mwaka mpya.
Taarifa zinadai kuwa Pardew alikuwepo kwenye dimba la mazoezi la timu
hiyo siku ya Ijumaa na sasa anakwenda kuwa mrithi wa menejaNeil Warnock
aliyetimuliwa siku ya Krismasi.