Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda wakizungumza na Mchezaji
Mwinyi Kazimoto ambaye ni Mtanzania anayecheza soka la kulipwa katika
timu ya Al Markhiaya nchini Qatar, katika mkutano kati yake na
watanzania waishio nchini humo uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton
mjini Doha Desemba 21, 2014.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda (kushoto kwake)
wakizungumza na baadhi ya washiriki wa mkutano kati yake na watanzania
waishio nchini Qatar uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo Doha,
Desemba 21, 2014. Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio
nchini Qatar baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Sheraton iliyopo
Doha, Desemba 21, 2014.