Wafanyakazi
wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo
cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono
jijini Arusha katika tam
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma.
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
Grace Joseph(12)wa kituo cha kiwohed akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa "NISEME"wimbo wa moto band
Mashindano yakiwa yanaendelea
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
Meneja ubunifu wa Redio 5
Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja
katika shindano la kucheza muziki
Meneja ubunifu wa Redio 5
Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili
baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
Meneja ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
Mtangazaji wa kituo hicho
Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na
watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
Wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa katika maandalizi ya kuwaandalia watoto mapochopocho
Kampeni ya ushindi ikiwa inaendelea huku watoto wakiwa wanancheza michezo mbalimbali
Wadau wakiwa wanafatilia shindano
Kulia ni mtoto Sharon
Nelson akiwa anakabidhi msaada alioleta katika kampeni ya ushindi
amewataka watoto wengine kujitolea kusaidia wasionacho
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo.
Kampuni Tan Communication Media inayo
miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha
imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina
"Kampeni ya USHINDI"linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa
Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho Robert Francis
anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya
kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione
kutengwa
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo
alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale
wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi
watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya
ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa
kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio
5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful
company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)