TIMU
ya Yanga veterani imeibuka mshindi wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba
veterani ulioandaliwa na PSPF, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 4-3 na
kubeba kombe. Mchezo huo ulifanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja
wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.
Hadi
dakika tisini zinakamilika timu hizo zilitoka sare ya bao moja kwa moja,
mabao hayo yaifungwa na Omari kapilima kwa upande wa Yanga na Barnabas
Sekolo kwa upande wa Simba.
Bingwa
wa mchezo huo alipatikana kwa njia ya matuta, ambapo kwa upande wa
Yanga walipata penalty ni Empram makoye, Ngada Shaganga, Ismail Issa na
Deo Lucas. Yanga ilikuwa ikifundishwa na Peter Tino Kasongo Athumani
kwa
Kwa upande wa simu waliozamisha penati ni Athumani Chama, madaraka
Selemani na Issa Manofu. Simba ilikuwa chini ya Kasongo Athumani.
Lengo
la mchezo lilikuwa kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na
maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa
mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo Mkopo
wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Kikosi cha Simba.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Simba.
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akizungumza na vyombo vya habari kabla ya
mchezo kuanza, kushoto ni Godfrey Ngonyani Mkurugenzi wa ukaguzi wa
ndani.
Simba wakipewa kombe lao.
Mabingwa wakipewa kombe lao.
Mabingwa wakiwa na kombe lao.
Mchezaji wa Simba akijiunga na PSPF.