KAMPUNI ya
usafirishaji ya Usangu Logstics Ltd,(Mwakabwangas), imejenga kivuko
kinachounganisha Tarafa za Ilongo na Rujewa, katika wilaya ya Mbarali mkoani
hapa.
wilayani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ibrahim
Ismail, alisema kuwa kampuni yake ilifikia uamuzi huo baada ya mwaka jana
kutembelea eneo hilo na kumuona Bibi kizee ambaye alikuwa akivuka kwa miguu ndani
ya maji huku akihitaji msaada.
Alisema hali
hiyo ilimgusa na kuamua kushirikisha uongozi wa kampuni yake na kuamua kufanya
upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kivuko hicho kisha kukitengeneza Jijini Dar es
Salaama na kupeleka wataalam wengine katika eneo hilo kwa ajili ya kukifunga na
sasa kimeanza kutumika.
“Tangu dunia
kuwepo, hakujakuwepo kivuko, lakini kivuko hiki kwa sasa kimekuwa mkombozi kwa
wananachi na ni sadaka yangu kwa Mungu kwa ajili ya kuhudumia watu hasa
wajawazito na wazee. Kina uwezo wa tani 25 na sahani ya kukalia, ina uwezo wa
kubeba watu nane na kimegharimu Shilingi Milioni 35” alisema Ibrahim.
Mbali na
kivuko hicho, alisema tayari ameanza ujenzi mwingine wa kivuko cha mto Barali
kitakachokuwa na urefu wa mita 100, kitakacho gharimu kiasi cha Shlingi Milioni
35.
Sambamba na
vivuko hivyo, alitembelea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbarali mwanzoni
mwa wiki hii na kuwapa pole kwa kuwapatia sabuni na kwamba alichokigundua ni
kwamba kuna uhaba wa vitanda vya wagonjwa.
Kampuni ya
(Mwakabwangas), kwa kutambua tatizo la maji safi katika wilaya hiyo, imechimba
visima vya kisasa katika maeneo ya Isisi, Utengule Usangu ambako ndiyo chimbuko
la kampuni hiyo na Ilongo, vinavyogharimu Shilingi Milioni 80 kwa kila kimoja.