
Milio
ya risasi imesikika na kuna ripoti ya kukamatwa kwa mateka mmoja huku
maafisa wa polisi wa Ufaransa wakiwazingira washukiwa waliohusika na
mauaji ya Charlie Hebdo.
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika eneo la Dammartin-en-Goele yapata kilomita 35 kutoka Paris,lakini maafisa wamekana ripoti ya mauaji yoyote.
Majadiliano ya polisi yanaendelea ripoti zimesema.
Mpango huo unajiri karibia masaa 48 baada ya shambulizi hilo katika afisi za gazeti hilo ambapo watu 12 waliuawa kwa kupigwa risasi.
